Habari za Karibuni : Dr. Kikwete : Atangazwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ni mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  |   Dr. Shein : Aibuka Mshindi Kwa Nafasi ya Uraisi Zanzibar Kwa 50.1%  |   Dr. Bilal : Afunika Pemba, Apata Mapokezi Makubwa  |   Dr. Bilal : CCM Government to Tap Skills From Tanzanians in Diaspora  |   Dr. Bilal : Aingiza CCM Wanachama Wapya 137 Korogwe  |   Dr. Bilal : Vunjeni Makundi Tupate Ushindi Mnono  |   Dr. Bilal : Aitabiria Makubwa Rukwa  |   Dr. Bilal : Avunja Ngome ya Upinzani Kagera Aingiza wanachama wapaya 144 CCM  |   Dr. Bilal Ampigia Debe Dr. Shein Awataka Wana CCM Kuacha Makundi  |   Dk. Kikwete : Tutawakopesha Wavuvi Zana za Kuvulia  |   Msichague Rais Kwa Majaribio - JK !  |   Do not gamble with your vote, says Kikwete  |   Bumbuli yafurika kwa mapokezi ya Kikwete  |   Dr. Bilal : Ahidi Kushughulikia Chuo cha ualimu Mpwapwa Kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha UDOM  |   JK Apata Mapokezi Makubwa Namanga  |   Dr. Shein pulls record crowd  |   Dk. Kikwete : Shinyanga Kupatiwa Huduma ya Maji Serikali Ijayo  |  

Dr. Mohammed Gharib Bilal - Uchaguzi Mkuu Tanzania 2010

Dr. Bilal - First Day

Dk. Mohammed Gharib Bilal Aaanza Kazi Ramsi November 08, 2010

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amewataka watumishi wa ofisi yake kujizatiti katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema kwa kufanya hivyo, watawezesha kupatikana mafanikio katika awamu ya pili ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Dk. Bilal alisema hayo alipozungumza na Menejimenti ya ofisi hiyo. Alisisitiza umuhimu wa watendaji na watumishi wa ofisi hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba, sheria na kuzingatia taratibu za mawasiliano ya kiserikali. Dk. Bilal aliwakumbusha kufanya kazi kama timu moja ya serikali na nchi moja. Alisema anatarajia kuona wanajituma kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, uwazi na kuendeleza heshima ya ofisi.

Ningependa kuona system (mfumo) inafanya kazi inavyotakiwa, utendaji rasmi unaoheshimu mtu na nafasi yake. Ninaamini sote tutajitahidi kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba, Sheria na taratibu zilizowekwa,î alisema. Aliwakumbusha watumishi hao wajibu wa kuelewa mfumo mzima wa utendaji wa serikali, ili aweze kufanikisha majukumu yake ya kumsaidia Rais Kikwete. Makamu wa Rais aliwaasa watumishi kuzingatia wadhifa, fursa na wajibu waliopewa katika kuendeleza maelewano mazuri yaliyopo katika ofisi hiyo.

Dk. Bilal alisema majukumu ya wizara za Muungano na Mazingira zilizo chini ya ofisi yake ni muhimu kwa mustakabali wa taifa, hivyo hawana budi kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia ujuzi, taaluma na uzoefu wao. Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ruth Mollel, aliahidi kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, sheria na utawala bora.

Aidha, Dk. Bilal alibainisha kuwa majukumu ya wizara mbili katika ofisi hiyo yaani za Muungano na Mazingira ni muhimu kwa mustakabali wa taifa na hivyo hawana budi kuwa makini katika utekelezaji wake huku wakizingatia ujuzi wao, taaluma na uzoefu wao.

“Mazingira ni suala muhimu, yanatugusa sote popote tulipo, hivyo, tunapaswa kuwa makini zaidi. Nchi yetu ni changa hatuwezi kukabiliana na changamoto zinazotokana na athari za mazingira.

Tuimarishe ujuzi wetu, uelewa wetu na uzoefu wetu katika suala hili hapa petu na kwa jirani zetu na kwingineko,” alifafanua.

Dk. Bilal aliwakumbusha watumishi wa ofisi hiyo wajibu wao wa kuelewa mfumo mzima wa utendaji wa serikali ili afanikishe majukumu yake ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Dr. Mohammed Gharib Bilal - Wengi Wamerudi CCM Jee Wewe?

       

Dr. Bilal - Lindi

Dr. Kikwete : Arejea Tena Ikulu

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Lewis Makame amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2010 kuwa ni Dk. Jakaya Kikwete kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).

Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yalitangazwa 05/11/2010 majira ya saa kumi jioni na Mwenyekiti huyo katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu , Makame alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.

Aidha Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basin a mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.

“Kwa kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2010.

“Mheshimiwa Kikwete Jakaya Mrisho amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Bilal Mohammed Gharib amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mwenyekiti huyo.< br />
Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 20,137,303, waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha, zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64 ya kura zilizopigwa.

Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36 ya kura zote zilizopigwa, hivyo Kikwete amepata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali.

Wagombea waliofuatia ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye ni Slaa Willibrod Peter amepata kuwa 2,271,941 ambazi ni sawa na silimia 26.34 ya kura zote halali, Lipumba Ibrahim Haruna wa chama cha CUF, amepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali, Mziray Kuga Peter wa APPT – Maendeleo amepata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12 ya kura zote halali.

Wengine ni Rungwe Hashim Spunda wa NCCR- MAGEUZI amepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31 ya kura zote halali, Mgaywa Muttamwega Bhatt wa TLP amepata kura 17,482 sawa na silimia 0.20 na Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa wa UPDP amepata kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali.

Akitoa salamu kwa niaba ya wenzake badala ya Slaa ambaye hakuwepo uwanjani hapo, Lipumba alimpongeza Kikwete na Makamu huku akisisitiza suala ya ushiriki wa watu katika kupiga kura liangaliwe na kusema Rais aliyeshinda ni Watanzania wote.

Alisisitiza suala la elimu bora , ajira, ujengaji wa miundombinu na uvumulivu wa kisiasa ni muhimu, hivyo alimshauri Rais Mteule Kikwete kujiwekea malengo katika kipindi cha miaka 5 ijayo, ambayo ni uongozi wa demokrasi, ujenzi wa uchumi ajira kuboresha miunbombinu, utawala na kupamban na rushwa.

Pia alimkabidhi Rais Mteule Kikwete Ilani ya chama chake kwa ajali ya kusaidia katika utendaji wake wa kazi.

Kwa Upande wake Rais Mteule Kikwete, alitoa shukurani za ushindi alioupata na kusema watazifanyia kazi changamoto zilizibuliwa wakti wa kampeni yakiwemo mawazo ya Lipimba.

Alivishukuru vyombo vya habari kwa tendaji wao wa kazi , lakini aliviomba kufanmya kazi zaidi ya kusaidia kutibu majeraha ya nchi ili kurejesha umoja na amani badala ya kuongeza chumvi.


Dr. Mohammed Gharib Bilal - Wengi Wamerudi CCM Jee Wewe?

       

Dr. Mohammed Gharib Bilal on the News

  1. Uchaguzi Webcast


Dk. Mohammed Gharib Bilal Akiwa Katika Mfululizo wa Mikutano ya Kampeni

 


Dr. Mohammed Gharib Bilal - Wasifu wa Mgombea Mwenza Urais 2010


Mohammed Gharib Bilal ,mwanasayansi wa nuklia alizaliwa Unguja mwaka 1945 na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi katika skuli ya Makunduchi, wilaya ya Unguja mwaka 1958. Elimu yake ya sekondari alipatia katika ya shule Beit-el-ras mwaka 1962 na kufanikiwa kuingia kidato cha tano mwaka 1963 katika skuli ya sekondari ya Lumumba, Zanzibar. Kabla ya kumaliza kidato cha tano alipata scholarship ya kwenda Marekani,ambapo alisomea masomo ya fizikia katika Chuo Kikuu cha Howard na kuhitimu shahada yake ya kwanza katika fizikia na hesabati mwaka 1967. Baada ya shahada ya kwanza alijiunga na Chuo kikuu cha Carlifonia kwa shahada ya juu kwenye Chuo cha Berkely na kupata shahada ya M.A Physics mwaka 1969. Baada ya kuhitimu alianza kazi kama msadizi wa elimu yaani, Teaching assistant. Mohammed Gharib Bilal alikuwa mkufunzi wa utafiti (research assistant) hadi mwaka 1976 alipofanikiwa kupata Phd ya fizikia kutoka Chuo Kikuu cha Carlifonia.

Baadae mwaka huohuo alijiiunga na Chuo kikuu cha Dar-es-salaam kama mhadhiri wa fizika katika kitengo cha fizikia. Mwaka 1983 alichaguliwa kuwa mkuu wa Idara na kuongoza kitengo cha Fizikia ya Nyuklia.Katika kipindi hicho aliwafundisha zaidi ya wanafunzi 10 kwenye masomo ya shahada ya uzamili. Mwaka 1983 alishiriki kuanzisha shirika la mionzi la Taifa kwa kuchangia kitaalamu maandalizi ya mswada ambao ulitupatia sheria ya udhibiti wa matumizi ya mionzi ya nyuklia nchini. Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mkuu wa Kitivo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na kuendelea katika wadhifa huo hadi mwaka 1990 alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara mpya ya wakati huo ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu mwaka 1990-1995.

Akiwa Katibu mkuu alishiriki katika kuanzisha utaratibu wa kuchangia gharama za elimu ya juu na kuanzisha utaratibu wa mikopo. Pia wizara hiyo ilianzisha Chuo Kikuu Huria , pamoja na kuanzisha udhibiti wa vyuo vya elimu ya juu ( accreditation council). Mnamo mwaka 1988 Dr Bilal alianzisha mradi wa science camp mjini Zanzibar iliyolenga kuwahamasisha vijana kusoma sayansi na kuzisaidia shule za sekondari zote za Zanzibar(Unguja na Pemba) Kupata vifaa vya kuwezesha kufanya majaribio ya wanafunzi ili waelewe zaidi sayansi kwa vitendo. Mradi huo hatimaye ulirithiwa na Wizara ya Elimu Zanzibar. Mradi huo uliwasisimua vijana wengi katika sayansi na kuwapa changamoto nyingi za kujifunza mada mbali mbali zilizogusa mazingira ya Zanzibar. Akiwa mwalimu wa Chuo Kikuu Dr Bilal aliweza kushiriki katika bodi mbali mbali, kama vile Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH), Tume ya mionzi (NRC), Mwenyekiti wa science panel ya Inter university council of East Africa na pia alishiriki kuasisi masomo ya juu ya mazingira katika sayansi(1990). Mohammed Gharib Bilal alipata fursa ya kuhudhuria semina na kozi fupi katika fani mbali mbali kwa mfano, semina za shirika la Atomiki (IAEA) 1980 Kwabena, Ghana. 1984/85. Fellowship chuo kikuu cha Singapore. Vilivile huudhuria vikao vya kila mwaka vya shirika la Atomic.

Mwaka 1995 Dr Mohammed Gharib Bilal aliteuliwa kuwa Waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi 2000. Na katika siasa Dr Bilali amekuwa akikitumikia Chama Cha Mapinduzi katika nafasi mbali mbali kama vile kuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa na Kamati Kuu tangu mwaka 1995 na pia amekuwa Mlezi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Mkoa wa Pwani. Dr Bilal alikuwa Mwenyekiti wa kutafuta utaratibu bora wa kura za maoni wa kuwapata wagombea katika chaguzi za Dola kwa tiketi ya CCM. Mwaka 2004, aliteuliwa na Chama kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Magazeti ya Chama. Mnamo mwaka 2007, Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete alimteua Dr Bilal kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dodoma.